Sunday, December 4, 2016

Huduma za kijamii

Samuel

Kama huduma Tunawapelekea neno la Mungu watu waishio katika mazingira magumu kama vile yatima, wajane, wafungwa na wazee.Tuna watembekea katika vituo vyao au sehemu wanazo ishi ambapo huwa tunapeleka ujumbe wa Mungu pamoja sadaka zetu hapo kama zawadi  tukifurahi wema wa Mungu pamoja nao.

Tunashiriki huduma zingime za kijamii ikiwa no pamoja na kujitolea kulipia  ada za wanafunzi, kuwanunulia vifaa vya shule, na mengine mengi.


 Karibu tujenge ufalme wa Mungu

Saturday, December 3, 2016

Maomni/maombezi

Samuel

Kutokana na mipaka ya kidini,kidhebu na kimila tunatambua kuwa wapo watu ambao hawawezi kuingia kanisani, jambo hili linawanyima kupokea vipawa vya Mungu wao ikiwa ni pamoja na kumtambua Mungu katika maisha yao.

Neno ministry hutoa huduma ya  maombi,maombezi, mafundisho na ushauri kupitia mtando,kwa njia hii tumewafikia wengi na wamepokea Baraka zao.Huduma za maobi na maombezi pia hutolewa kwa kuonana na mhusika ikiwa atapenda kufanya hivyo.Hiduma hii hutolewa pasipo malipo ya aina yoyote ile.
Samuel

Tunamshukuru Mungu kutujalia neema ya kuyafika maeneo mbalimbali ya nchi yetu kwa ajili ya semina . Semina hizi huandaliwa kwa kushirikiana na umoja wa makanisa au kanisa moja wapo mahali semina hufanyika.

Mara nyingi gharama za kuendesha semina hubebwa na huduma ya Mkate hai ministry isipokuwa ukumbi ambao huwa ni kanisa litakalo pendekezwa na umoja huo au kanisa litakalo shiriki pamoja nasi kuandaa semina.

Pamoja na kufanya semina,pia huduma imekuwa ikitoa watumishi kwenda kuhudumu ibaada za kawaida au kufundisha semina katika kanisa litakalo hitaji Huduma ya mafundisho au mahubiri, huduma hii hutolewa pasipo malipo yoyote

Jifunze kila mahali

Samuel

Neno ministry ni rafiki yako wako wa karibu anaye kupenda sana na kuudhihirisha upendo huo kwa kucuatana nawe popote ulipo na saa yoyote yupo nawe karibu.

Katuka ulimwengu wa Leo tumezungukwa na mambo mengi yenye changamoto kubwa katika maisha yetu zimazo tishia ustawi wetu wa kiroho na kimwili hivyo tuna hitaji upendo, amani na kumtegemea Mungu kwa kila jambo ili tuweze kukua kiroho na tuwe na afya njema kimwili.

Neno ministry inalitambua hilo, hivyo kwa msaada wa Roho mtakatifu imeamua kwa dhati kukuletea mafundisho ya kiimani uenye kupa elimu ya kukusaidia kudhikabiri changamoto hizo bila kujali ubali au muda gani tutakuwa nawe popote ulipo.

Sasa waweza kufuahia na kushangilia katika Kristo Yesu ukiwa na simu yako au Kompiter yako mahali ulipo kwa kushiriki mafundisho haya, maombi na maombezi au sadaka wakati wowote.

  Kuwa mmoja sasa wa wale.wamgojao

Ushirika wa imani

Samuel

Neno ministry inaamini katika kushirikiana na waamini wengine katika Imani yenye msingi katika Kristo Yesu aliye Jiwe kuu la pembeni 
(Mathayo 21:42 "...Jiwe walilolikataa waashi, Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni; ...")
katka ujenzi wa ufalme wa Mungu.

Tunatambua kuwa hatupo peke
yetu bali wapo watumishi wengine waliojaliwa neema ya kujenga katika msingi huu imara. Kama Yesu alivyo sema Luka 9:50
".. Msimkataze, kwa kuwa yeye ambaye si kinyume chenu yu upande wenu ".

Ni katika msingi wa andiko hilo  tunashirikina na huduma zingime, makanisa na watu bimafsi waamini na walio tayari kujenga ufalme wa Mungu kupitia mafundisho ya kweli ya Biblia chini ya uongozi wa Roho mtakatifu. Tunaamini hii ndiyo njia pekee ya kushirikishana vipawa hata mwili wa Kristo upate kujengwe.
Waefeso 4:12
"kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe;"

Kusaidia wengine

Samuel

Kama ilivyoandikwa katika maandiko matakatifu like kitabu cha Math.10:8 "mmepata bure, toeni bure ". Tunatoa bure vipawa, muda na fedha  zetu tulivyopewa kwa neema tuu na Mungu baba kuwasaidia wenye uhitaji. Tunafanya hivyo si kwa sababu tuna vingi sana hapana Bali ni kwa sababu ya pendo alilotupa Yesu mioyoni mwetu.

Tunajua kuwa tulicho nacho ni kidogo lakini twakusihi ukipokee hicho tunajua Mungu ataki ariki hata kiwe Cha baraka. Matendo ya Mitume 3:6 "...akasema, Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende ". Tunaomba upokee na kitunze kwa ajili ya wengine.



Tunakusihi ungana pamoja nasi Leo katika kuwasaidia wengine usisisema sina kitu toa hicho ulicho nacho kwani wako wanao kihitaji hicho kiwasaidie.Njoo umpe Mungu utukufu kwa kugusa maisha ya weingime, kwani ulizaliwa ili kusa abisha tabasamu katika nyuso za wanao kuzunguka.