Jiunge na maelfu wamgojao Bwana.

Neno liatadumu milele

Kwa mkristo kuishi bila kuonba ni sawa na kutaka ushi bila kupumua,utakufa tu

Mafundisho ya kibiblia

Tuesday, January 28, 2020

Mwambie Mungu asante

Samuel
Mwambie Mumgu asante Kwa wema wake kwako hata kama hujui ni kitu gani amekutendea we mwambie asante kwani kuna mengi ametenda bahati mbaya macho yako hayaoni.

Biblia ina tushari kumwambia Mungu asante Kwa kila hali tunayo ipitia maishani mwetu hata kama ni hatua chungu kwetu lakini inatupasa kujua kuwa Mungu amefanya hayo Kwa sababu anatupenda na no Kwa Tunafaida yetu wenyewe, tunasoma 1 Wathesalonike 5:18
[18]shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.

Aisee mwambie Mungu asante!.

Mungu anasema 1 Petro 5:7 [7]huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.

 Ndiyo Mungu hujishughulisha Sana nambo yako, Ile kwamba hauoni haimanishi hajisghulishi na mambo yako jua bado anahangaika Sana kuhakikisha unapata mahitaji yako.

Angalia Leo hii Una mwaka hujafika hospital kabisa nawe ni shahidi ukienda hospital Una kuta watu wamelala hawajiwezi unadhani wewe ni mjanja kukwepa bacteria wa magonjwa hata uwe mzima Leo hii?.

Aisee mwambie Mungu asante.

Tazama Vizuri ona wapendwa wametwaliwa pikipiki zimewapitia lakini wewe kila siku wapanda pigipiki je ni kweli mpaka hapo huoni cha kusema asante Kwa Mungu wako. haikubaliki kabisa hebu kuwa Makini kidogo mwambie Mungu asante.

unajua wakati fulani unaweza kudharau kitu lakini usijue Mungu amehangaika mmno mpaka wewe ukapata japo hukidhamini. Biblia inatupa mfano mmoja mzuri Sana unao patikana katika 1 Wafalme 17:5-6
[5]Basi akaenda akafanya kama alivyosema BWANA; kwa kuwa akaenda akakaa karibu na kijito cha Kerithi, kinachokabili Yordani.
[6]Kunguru wakamletea mkate na nyama asubuhi, na mkate na nyama jioni, akanywa maji ya kile kijito.

Hii nu habari ya Eliya hebu tutafakari pamoja tuone jinsi Mungu anavyojishughulisha na maisha yetu. Ona kulikuwa na njaa Kali Sana kiasi kwamba Mito ilikuwa imekauka sasa jiulize hivi kungulu aliutoa wapi ule mkate na Ile nyama kila siku. Halafu Kwa nini kungulu mwenyewe hakula ikiwa kulikuwa na njaa nchi zima, je Nani huyu alikuwa pole na shibe nyingi kiasi cha kutupa mkate na nyama kila siku?. Nini naona hapa ni kuwa kile chakula hakikuwa cha kimwili hapana Bali kiliandaliwa na Mungu mwenyewe si unakumbuka aliwahi kuwapikia waisraeli Mana jangwani. Tena kumbuka kuwa Elia aliwahi kuletewa mkate na gudulia la maji na malaika ( 1 Wafalme 19- 8 ) Kwa hiyo usishangae nikikuambia Mungu alimwandalia Elia chakula na kujifikisha kwake Kwa njia ya kungulu.

Hallelujah!. Eliya angeweza kudharau kile chakula ukizingatia kimeletwa na kungulu,sote tuna mfahamu vizuri kungulu kuwa si msafi, Eliya angewza kusema Mimi ni mtumishi mkubwa wa Mungu siwezi kulishwa na kungulu lakini tunaona Eliya alipokea Kwa shukrani.

Mpendwa inawezekana kweli umelalia vipande vya mhongo nawe Una maswali kwanini ule mihongo wewe ni mtumishi,  sikia ndugu yangu mwambie Mungu asante hata Kwa hiyo mihogo maana Mungu amehangaika Sana kuhakikisha wewe unaipata hiyo mihogo nakwambi mwambie Mungu asante. kuna watu hata mhogo wamekosa siku ya Leo.

jifunze kumwambia Mungu asante atakubarikia mihogo yako utashangaa, pengine hunielewi angalia mezani kwako Leo Una ungali na matembele tuu lakini Kwa jirani yako mezani kuna mbonga Saba na matunda kibao na ni kila siku lakini ajabu ni kwamba wewe Una afya Bora kuliko yao, unaelewa lakini ?,mwambie Mungu asante. Rafiki jirani yako ana gari zuri lakini angalia jinsi wanavyo gombana kila siku lakini wewe na mwenza wako mnajipia kiwali chenu tena hata mafuta hamna  mwaongaza kanisani , mara sokoni mna Amani Tele mioyoni j
huoni kuwa ni ajabu.

Asisee mwambieesu asante.

kuna wakati mwingine Mungu anawainua watu hata Wale ulifikiri hawazi kukusaidia Kwa sababu hawana uwezo. Hebu angalia kisa cha Elia kutunzwa na Yule mama mjane. Utakubaliana NAMI kuwa si Jambo la heshima mwanaume mzima kutunzwa na mwanake tena mjane haiingii akilini kabisa tena Kwa upande wake Eliya alikuwa nabii ambaye Mungu aliweza kujibu maombi yake Kwa Moto lakini Mungu aliruhusu atunzwe na mwanamke mjane sijui unpo  jaribukukaa mahali pa Eliya unajiaikiaje wewe lakini kwangu maswali ya Yuko wapi Mungu ninaye yemtumikia yasimgekosekana. Eliya aliyapokea haya yote Kwa shukrani.

Mpendwa kuna mengi sana ambayo Mungu anafanya katika maisha yetu hata hatuelewi Kwa nini amefanya Kwa sababu tunaona either ametuonea au hatukustahili tutendewe vile sababu Sisi n Wana wa ufalme lakini Biblia inatuambia yeye Mungu amejishughulisha Mno na maisha yetu mpaka tuko hivi.ni Kwa kulijua hili ndio maana Biblia umetushauri tumahukuru Mungu Kwa kila Jambo maishani mwetu.

Mwambie Mungu asante.

Katika jina la Yesu nasema na wewe sasa ambaye umeachwa na mchumba wako futa machozi mwambie Mungu asante iko nguvu katika kushauru utaona Mungu akigeuza machozi yako kuwa kicheko kumbuka wale 10 wenye ukoma mmoja wao alipo Rudi kushauru akapokea uponyaji kabisa wa mwili wake. Iko nguvu katika kushauru nasema nawe uliye fell mhtihani wako na sasa umebaki kumlaumu Mungu nakuambia Kwa kina la Yesu geuka!. badili mtazamo wako Anza kusema asante Kwani iko njia amekuandalia utafika chuoni tu. Inuka Baba inuka mama  mmekosa mtoto muda mrefu mmesikia maneno ya kila namna Sawa lakini leo neno hili lifanyike unabii kwako badili kilio chako kiwe shukrani Yesu atafanya zaidi ya uwazayo wewe. Hilo lililo mbele yako ni  kweli ni  kubwa lakini bado Mungu hajashindwa

MWAMBIE MUNGU ASANTE!.

Thursday, December 19, 2019

Samuel
IdeaPad ni moja wapo ya bidhaa inayo tengenezwa na kampuni ya Lenovo inayojishughulisha na utengenezaji wa kompyuta ikiwemo Ideapad s125. kama ilivyo Kwa bidhaa nyingine kadhalika IdeaPad s145 ipo sokoni, inapatikana Kwa urahisi katika nchi nyingi duniani kupitia mtandao wa Amazon. Ukitazama tu bei yake utapata tariifa flani kuhusu Lenovo s145. Kama uonavyo bei yake ni ya chini Kwa hiyo usitegemee laptop hii kumfanya majukumu mazito ya kikompyuta kwani imeundwa maalumu Kwa ajili ya kazi za kawaida na si vingine, hata hivyo haina maana kuwa haiwezi kumfanya majukumu mazito unaweza lakini si Kwa ufanisi mkubwa, ushauri wetu wa bure ni vema itumike katitka majukumu ya kawaida.

Full story.

Design

Laptop hii ni mzuri na ya kuvutia Sana kuitazama, ni nyepesi na ina uzito usio zidi 1.45Kg pia ni nyembamba. Sifa hizi huifanya uweze kwenda nayo mahali popote bila kuhisi kama kuna kitu umebeba mgongoni kwako. Siku hizi nasikia unapo nunua unapata na begi lake bure, unaweza kupata tarifaa kamaili kuhusu mabegi ya Lenovo Kwa kuongia hapa.

Processor

Lenovo IdeaPad s145 inatumia celeron or pentium processor, Kwa mantiki hiyo huwezi run demanding Apps au kumfanya majukumu mazito ya kikompyuta kama nilivyo Sema hapo awali. Lakini kwa mtumiaji wa kawaida hii ni laptop mzuri sana ambayo huhitaji kuvunja bank yote ili uweze kuipta Laptop hii,inafaa Sana hasa Kwa waanafunzi ukiondoa Wale wa kozi za engineering na multimedia ambao wakati mwingine huhitaji high resolution au run demanding Apps.

Display

Ingawa display yake ni kubwa (15.6inch) ambyo ni display nziuri Kwa matumizi kama kuangalia movie au kucheza game (gaming), ukweli ni kwamba display hii ina tatizo la resolution Kwani ina resolution 1366x768 ambayo si resolution nziuri Kwa matumizi ya gaming hata ukiiangalia viewing angle yake si nziuri.

Sound


CPU.

Ingawa kuna uwezekano wa upgrade toka IdaPad ya kawaida na kuwa kama Toleo la gharama la IdeaPad 145 inayo tumia i7 processor inayo kupa rocket boosting speed,hasara yake ni kwamba utalazimika kulipa zaidi na mwisho wa   siku  bado unapambana na matatizo kadhaa ikiwemo poor resolution na pia kuna uwezekano wa  battery yako uwezo wake kushuka Sana.

Storage.

Laptop mpya inakuja storage ya 1TB, hii ni habari njema Sana Kwa kuwa Una kuwa umepata storage kubwa utakayo weza kukidhi matumizi yako. Habari mbaya no kwamba ina 5400rpm hard disk Jambo linalo ifanya loading time yake kuwa ndefu hasa unapotaka run Apps au kutafuta mafaili.Kumbuka kuwa inawezekana kuupgrade speed yake wewe mwenyewe nyumbani Kwa kwako Kwa kufungua screw chache na kupachika RAM mpya lakini tunapenda kushauri usifanye hivyo watagute watu wenye uzoefu wakusaidie ikiwa unawazo la kuiongezea speed laptop yako.

Bottom line.

katika uchunguzj wetu tumebaini kuwa Laptop hii ni mzuri ukilinganisha na bei yake. Hivyo tuna shauri kwa mtumiji wa kawaida no vema ukajipatia Lenovo s145 utaokoa pesa yako na bado ukafanya kazi zako Kwa ufanisi mkubwa. Tuna amini hutasita  kutushukuru baadaye. Inapatikai maeneo mengi na moja wapo ni katika Amazon  ambapo kwetu ni mahali salama kabisa kwa manunuzi yako, on purchase Laptop hii inakuja na adapter yake lakini pia unaweza kujipatia vifaa vingine mhimu katika kuboresha utendaji wa Laptop yaka kama vile external memory na vingine ambavyo unaweza kubapata Kwa gharama nafuu kupitia kiungo hiki Lenovo s145 accessories.

Sunday, December 8, 2019

Mchungaji mwema

Samuel

Shalom kanisa!
Mchungaji mwema:
Leo naomba tuangalie  neno hili la mchungaji.yupo mchungaji mwema wa Roho za watu na mchungaji mwema wa
ng'ombe. Nami nataka tumwangalie yule wa ng'ombe tupate kuelewa vema.

Ni jukumu la Mchungaji wa ng'ombe huyu ndiye anaye jua wapi mifugo yake itapata malisho lakini ng'ombe(mifugo) wenyewe hawajui, huwa anafanya bidii kuwaongoza  g'ombe wake wafuate njia lakini ng'ombe wenyewe hawajui njia. Mchungaji wa ng'ombe yeye hujua sana afya ya mifugo wake. Kwa kweli ng'ombe humtegemea yeye kwa kila kitu.

Nimepata kutafakari juu ya ng'ombe nilipo kuwa nikisoma maneno haya 

John 10:1-5
[1]Verily, verily, I say unto you, He that entereth not by the door into the sheepfold, but climbeth up some other way, the same is a thief and a robber. 
Yesu aliwaambia, Amin, amin, nawaambieni, Yeye asiyeingia mlangoni katika zizi la kondoo, lakini akwea penginepo, huyo ni mwivi naye ni mnyang’anyi.
[2]But he that entereth in by the door is the shepherd of the sheep. 
Aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo.
[3]To him the porter openeth; and the sheep hear his voice: and he calleth his own sheep by name, and leadeth them out. 
Bawabu humfungulia huyo, na kondoo humsikia sauti yake; naye huwaita kondoo wake kwa majina yao, na kuwapeleka nje.
[4]And when he putteth forth his own sheep, he goeth before them, and the sheep follow him: for they know his voice. 
Naye awatoapo nje kondoo wake wote, huwatangulia; na wale kondoo humfuata, kwa maana waijua sauti yake.
[5]And a stranger will they not follow, but will flee from him: for they know not the voice of strangers. 
Mgeni hawatamfuata kabisa, bali watamkimbia; kwa maana hawazijui sauti za wageni.

Kwa kweli nikawa silewi ndipo nilipoomba msaada wa Roho Mtakatifu anisaidie kuelewa, baada ya ombi hili nikaletewa picha ya ng'ombe na ndiyo sababu mimetumia ng'ombe badala ya kondoo.

Sasa twende pamoja, Yesu ndiye mchungaji mwema , Japo si neno njema lakini nakuomba ukae mahali pa ng'ombe upate kuelewa vema

Unajua ng'ombe ni msumbufu sana kwa kuwa hajui atakula wapi hivyo mchungaji ng'ombe tu ndiye ajuye na huamua wapi ampeleke ng'ombe wake akale hata hivyo ng'ombe hafuati njia bali hutoka katika njia na kutaka kula mazao ya watu mchungaji wa ng'ombe hulazimika kumkataza asiharibu mazao ya watu kwa kuwa anakompeleka kuna malisho bora ya hayo lakini ng'ombe haelewi na hukasirika.

Hivi ndivyo tulivyo,hatujui kesho yetu wala ridhiki zetu zilipo ni Mungu pekee ajuauye naye hutuongaza palipo malisho mema.

Psalms 23:2
[2]He maketh me to lie down in green pastures: he leadeth me beside the still waters. 
Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza.

Hata hivyo hatuelewi tunakimbilia mambo mengine nje ya njia ya Mungu ( kusudi ) mbaya zaidi hata akitutaza tunakasirika! Eeh Yesu turehemu.

Ng'ombe hajui hata kusafisha mahali anapolala ni kazi ya mchungaji wa ng'ombe kusafisha zizi lakini wakati mchungaji wa ng'ombe anasafisha banda(zizi), ng'ombe mwenyewe wakati mwingine hupinga mateke kumbe usafi ule ni kwa faida yake, nasi ndiyo tulivyo Roho wa Mungu  anapotaka kutusafisha tuwe safi kusudi uchafu ( dhambi ) usije tuletea maradhi kisha kifo tunakasirika na kumsimanga Kwa maneno magumu ya kweli na sharau kuu.

Romans6:23
[23]For the wages of sin is death; but the gift of God is eternal life through Jesus Christ our Lord. 
Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu. Yesu tuhurumie.

Yesu ni mchungaji mwema huingia mlangoni na mifungo yake humfurahia naye huwafungulia mlango humfuta,naam Yesu ni mchungaji Wa kweli ndiyo maana huja kwako kwa upole na kukueleza juu ya kusudi lake umtumikie wala hakulazimishi umtumikie.

Revelation 3:20
[20]Behold, I stand at the door, and knock: if any man hear my voice, and open the door, I will come in to him, and will sup with him, and he with me. 
Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.

Bali shetani kwa kuwa ni mwizi haipiti mlangoni ndiyo maana anakulazimisha ufanye atakayo wala hakuombi. Changua leo kuwa upande Wa mchungaji mwema au mwizi, lakini sisi Neno ministry tunakushauri chagua upande wa  Yesu.

Nataka ufahamu leo kuwa kama ilivyo kwa mchungaji wa ng'ombe, ndiyo ilivyo kwake Yesu mchungaji mwema,hujishughuliaha sana ili kuhakikisha unapata malisho nyakati zote.
Psalms 23:5
[5]Thou preparest a table before me in the presence of mine enemies: thou anointest my head with oil; my cup runneth over. 
Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika.

Ndiyo usiogope ana Huruma sana namfahamu vizuri kwani amesema mwenyewe kuwa

John 6:37
[37]All that the Father giveth me shall come to me; and him that cometh to me I will in no wise cast out. 
Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe.

Kama ilivyo kwa ng'ombe wala hajui atakula wapi kesho wala atatibiwa na  nani lakini yeye siku zote humwamini bwana wake wake atampeleka palipo na na malisho pia hata bwana wake akichelewa hupiga kelele kuomba msaada apelekwe panapo malisho.

Kadhalika nawe weka Imani yako kwa Yesu kuwa atakupa unacho hitaji hata kikichelewa piga kelele kwa njia maombi atakuja na kukupa hitaji lako.

Jifunze kumsubili Mungu anaye JIBU maombi hata kama litachelewa ujue ni kwa faida yako limechelewa au haja kupa.

Ushuhuda.
Mimi mwenyewe ni mtu niliyepata Neema ya kwenda shule ya juu, nakumbuka wakati naenda chuo mara ya kwanza niliomba mkopo sikupata japo nilikuwa na sifa zote za kupata mkopo, nilikasirika sana kwa nini Mungu hakurusu nipate mlopo. Japo hakunipa sababu lakini alinisaidia kuendelea na masomo yangu na nilifanikiwa kumaliza. Nilirudi chuoni tena na nikaomba mkopo lakini pia si kupata hapo nilazidi kuchukia na kumchukia sana Mungu, Mungu akaa kimya asinijibu why. Kwa shida Sana nilifanikiwa kumaliza chuo. Baada ya kurudi mtaani nikaaa miaka mingi bila kuwa na kazi ya maana, siku moja rafiki yangu akaniambia anadaiwa million 15 na bodi ya mikopo deni limejilimbikiza. Usiku ule nikitafakari juu ya deni la rafiki yangu ndipo Roho Wa Yesu akaniambia "Je ninge kupa ule mkopo ungelipaje?. japo ulinikasirikia sana lkn nilijua yaliyoko mbele yako nikazuia usipate mkopo kwa kuwa nakuwazia mema"

Jeremiah 29:11
[11]For I know the thoughts that I think toward you, saith the LORD, thoughts of peace, and not of evil, to give you an expected end. 
Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.

Hapo ndipo nilipo jua kuwa mawazo mema ya Mungu ni tofauti na vile ninvyo fikiri Mimi, tangu siku hiyo nimejua kuwa kila alifanyalo Yesu kwangu ni jema hata kamaa lina maumivu kwangu najua amelifanya kwa kuwa ni njema machoni pake na hii ni kwa ajili ya faida yangu.

Mpendwa hakuna mchungaji mwema anayeitakia mifungo yake madhara Bali yeye yu tayari kuutoa uhai wake kwa ajili ya mfugo wake.hivi ndiyo Yesu afanyanyvo kwako.akikuzuia jambo usikasirike Bali mshukuru kwa kuwa amefanya hayo kwa faida yako.

Kumbuka kuwa mawazo yetu si yake Mungu na tena mazo yake yako juu sana kuliko mawazo yetu.

Katika yote fahamu kuwa anakuwazia mema wala so mabaya.


Saturday, December 8, 2018

Nani aombe toba?.

Samuel

Shalom kanisa!.
Leo napenda tutazame japo kidogo juu ya toba kwa sababu ya ufinyu wa ukrasa wetu huu,tutaangalia mambo machache tuu Lakini nikiamni Roho wa Bwana atakuwezesha kujifunza ktk muda wako wa spare.

Toba kwa lugha nyepesi kabisa Ni kugeuka yaani kumgekukia Mungu wako na tunaposema kuomba Toba Ina maana ya kufanya maombi ya kutaka  kumsihi Mungu atusaidie tumgeukie yeye katika maisha yetu haya.

Nimezigawa Toba ktk mafungu mawili:

Moja:
Ni Toba inayofanyika unapokoka au unampokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako Toba hii Ni zao la Roho mtakatifu. Tunasoma kuwa 

2 Wakorintho 7:10
[10]Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba liletalo wokovu lisilo na majuto; bali huzuni ya dunia hufanya mauti.

Toba ile tulioimba wakatu tunamkiri kristo haikutokana na ushawiashi wa mwanadamu Bali ilikuwa kazi ya Roho Mtakatifu iliyofanyika ndani ndiyo iliyotuo goza hata tukamkri Kristo na hata tukapokea kipawa Cha wakovu.

Warumi 10:9-10
[9]Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.
[10]Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.

Ni tendo linapofanyika mara moja mtu husamehewa dhambi na kuhesabiwa haki na kumpokea wokovu, huanza Toba, Kisha hufuata kusamehewa dhambi,kuhesabiwa haki na Kisha kupata wokovu.

Mhimu kujua kuwa sio Toba inayotuhesabia haki bali ni Imani katk krsto Yesu, Mungu anaiona hiyo Imani ndani yetu hutuhesabia haki bure kwa njia ya neema maana neema ni kitu mtu hupewa bure pasipo kuifaniya kazi 

Warumi 4:4-5
[4]Lakini kwa mtu afanyaye kazi, ujira wake hauhesabiwi kuwa ni neema, bali kuwa ni deni.
[5]Lakini kwa mtu asiyefanya kazi, bali anamwamini yeye ambaye amhesabia haki asiyekuwa mtauwa, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki.

Toba hii tukiomba ikiwa na lengo la kusihi Mungu atusikie kilio chetu kuwa tumetambua kuwa tuko mbali na uwepo wake katika maisha yetu na kwamba Sasa tunamwitaji yeye awe kiongozi katika maisha yetu zaidi Sana tupewe neema ya kuingia katika ufalme wake 

Mbili:

Ile kwamba umeoka haina maana kuwa umefika Mbinguni hapana Bali unapewa tiketi ya kuingia ktk ufalme wa pendo la Mwana wake yaani ufalme wa Mungu. Ndiyo kwanza unaza safari ya kuelekea uzimani, kwa hiyo usifikiri Ni kazi rahisi ni ngumu kusafiri ktk njia hii. Hii Ni kwa sababu njiani utakutana na mtu mwe hasira sana

1 Petro 5:8
[8]Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.

Anatafuta Sana wa kunijaribu na anajitahidi kwa kweli kuhakikisha amekuweza kabisa si njia rahisi hii 

Ufunuo wa Yohana 12:10
[10]Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.

Lengo lake kuu apata Cha kukushitaki mbele za Mungu yaani asipo pata huumia Sana maana ndiyo kazi yake. Kwa hiyo usijaribu kumwona shetani Kama nidiyo chanzo kuasi kwako nakwambia mwezio alikuwa kazini apate Cha kusema.kwa hiyo Jifunze kuwambia kweli baba kuwa umemkosea akusamehe na sio visingizio juu ya ahetani au kusema Ni kwa sababu ya udhaifu was mwili hapana kwani Mungu alipokuambia usitende dhambi alikuwa anajua kabisa kuwa una mwili wa udhafu napia alijua shetani yupo duniani. Visingizio havitatusaidia tukumbuke visingizio vya Adamu havikumsadia kitu.

Ndugu yetu Paulo aliliona Hilo kwamba pamoja na kuwa mwongofu bado alikuwa katika mapambano ya dhambi yaliyo sababishwa na mwili wake mwenyewe amesema

Warumi 7:15-24
[15]Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda.
[16]Lakini kama nikilitenda lile nisilolipenda, naikiri ile sheria ya kuwa ni njema.
[17]Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu
[18]Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati.
[19]Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo.
[20]Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.
[21]Basi nimeona sheria hii, ya kuwa kwangu mimi nitakaye kutenda lililo jema, lipo lililo baya.
[22]Kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani,
[23]lakini katika viungo vyangu naona sheria iliyo mbali, inapiga vita na ile sheria ya akili zangu, na kunifanya mateka ya ile sheria ya dhambi iliyo katika viungo vyangu.
[24]Ole wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?

Mara kadha utu wetu wa ndani unatamani sana kufanya yaliyo ya Mungu lkn mwili hutupinga na tunajikuta tumefanya lile tunalo lichukia. Biblia ipo wazi hapa kuwa ikiwa tunalifanya tusilo lipenda basi dhambi iliyo ndani ya miili yetu ndiyo inayoa sabibisha 
Iwe hivyo. Fahamu kuwa miili yetu inaitikia kwa urahii zaidi mambo ya dunia kuliko ya Mungu hii ndiyo vita kubwa tuliyo waamini kuliko hata kupambana na nguvu za giza, tunasoma kuwa

Mhubiri 7:20
[20]Bila shaka hakuna mwanadamu mwenye haki hapa duniani, ambaye afanya mema, asifanye dhambi.

Ni kwa mantiki hiyo Mungu anatambua ugumu safari yetu ndiyo maana aliruhu iwepo toba tunapo anguka ktk hila za jamaa huyu.Biblia inatutaka kila wakati tuombe Toba mara tuangukapo dhambini. Tunasoma

1 Yohana 2:1-2
[1]Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki,
[2]naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote.

Biblia Inatuagiza tufanye bidii tusianguke dhambini kabisa,hata hivyo inatuambia kuwa ikitokea tumeanguka haraka tukumbuke kwenda kwa Yesu kuomba Toba yaani kusamehewa dhambi zetu kwa kuwa yeye ndiye mpatanishi Kati yetu na Mungu. Soma  vizuri inasema dhambi zetu yaani waamini na za ulimwengu yaani wasio amini.

 Ni kwa kutambua hilo Yohana  ansema
1 Yohana 1:8-10
[8]Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.
[9]Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.
[10]Tukisema kwamba hatukutenda dhambi, twamfanya Yeye kuwa mwongo wala neno lake halimo mwetu.

Angalia tuziungama dhambi zetu yaani sisi yeye ni mwanifu na wa haki atatusafisha, Jua imepasa tuungame yaani tusema samahani  tumekosa mbele zako, tuonyeshe kwa dhati kwamba tumesigitishwa na tulio yafanya,kuwa tunayachua hayo,kuwa hatuyataki, Yesu huisikia Toba yetu Kisha huenda mbele za baba yake kutuombea msamaha.

Mfano 1.
Kanisa la efeso liliwahi kupotoka katika njia yake ya kwanza (upendo) na kujikuta lipo katika nja mpya,Yesu alilikemea kwa kulitaka litubu mara moja

Ufunuo wa Yohana 2:5
[5]Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu.

Kwa hiyo tuba katika maisha ya mwamini Ni mhimu Sana kwa kuwa dhambi ni uchafu was kiroho. Katika ulimwengu Ni vigumu kutochafuka hata ukijifungia chumbani utajikua unachafuka tuu na vumbibhivyo lazima uoge uwe safi.kadhalika dhambi hutja hata Kama umjifungia nyumbani mwako bado dhambi itakujia tuu kwa kuwa dhambi haitoki nje tuu Bali wakati kwingine hutoka katika mawazo ya mioyo yetu.hivyo Ni mhim kwetu kila wakati kwenda ziwani mwa damu ya Yesu tukaoge tuwe Safi ili tuweze kusimama mbele za baba yetu was Mbinguni kwa ujasiri mkuu vinginevyo tutajificha tuu Kama Adamu kwani tutaona aibu ya uchi wetu kiroho 

JUA HILI PIA
Tuomba Toba pia ili tusipatwe na madhara yatokanayo na dhambi

Jambo unalopaswa kujua pia Ni Hili kuwa ikiwa tutatenda dhambi Mungu hafurahishwi nasi kwa hiyo huamua kuturudi kusudi tusipotee kabisa.

Waebrania 12:6-13
[6]Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, 
Naye humpiga kila mwana amkubaliye.
[7]Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye?
[8]Basi kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali.
[9]Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawastahi; basi si afadhali sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi?
[10]Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake.
[11]Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani.
[12]Kwa hiyo inyosheni mikono iliyolegea na magoti yaliyopooza,
[13]mkaifanyie miguu yenu njia za kunyoka, ili kitu kilicho kiwete kisipotoshwe, bali afadhali kiponywe.

Biblia inatuambia kuwa ili kusiwepo kurudia kwa kuwa kurudiwa ndani yake Kuna adhabu ambayo sio kitu Cha kufurahia, basi tukaifanye miguu yetu imara ( isihame katka nja iliyo sawa) ili kufanya njia iliyonyoka ili kilicho kiwete ( kisicho faa) kinyoshwe

Mfano 1.

2 Samweli 12:13-14
[13]Daudi akamwambia Nathani, Nimemfanyia BWANA dhambi. Nathani akamwambia Daudi, BWANA naye ameiondoa dhambi yako; hutakufa.
[14]Lakini, kwa kuwa kwa tendo hili umewapa adui za BWANA nafasi kubwa ya kukufuru, mtoto atakayezaliwa kwako hakika yake atakufa.

Daudi alipo mwambia Nathani nimefanya dhambi unaona jibu la Nadhani Ni Hili Mungu ameiondoa dhambi yako. Unaona hapa jibu Hilo halikuwepo kabla Daudi hajakiri kumtenda Mungu dhambi na usifikiri kuwa Daudi hakujua kuwa alilo fanya Ni dhambi alijua na ndio maana alitaka kuficha iwe Siri.Mtoto alikufa si kwa sababu ametenda dhambi hapana bali ni matokeo ya dhambi ya Daudi. Ni Toba pekee inayo weza kuzuia madhara ya dhambi.kumbuka Toba ya Musa juu ya Israel walipo abudu ndama.

Na HILi
Toba Ina mpa kibari Mungu kuwa upande wako au eneo unaloombea Toba. Fahamu kuwa ulimwengu wa Roho ni ulimwengu unaongozwa kwa sheria.maandiko yanatuambia

Warumi 8:2
[2]Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.

Kwa hiyo ipo Sheria ya uzima na ndiyo inampa Mungu uhali wa kuwepo au kushughulikia Jambo flani katika maisha ya wanadamu,Sasa hii haimanishi kuwa hawezi kufanya chochote mpaka vigezo vya Sheria hii vitimia kumbuka yeye  juu ya Sheria zote anaweza lkn hii Ni nje ya utaratibu alio jiwelea. 

Usisahau kuwa shetani anafanya kazi ktk mnyororo was dhambi Ni Sheria ya dhambi inayompa shetani kibari Cha kutawala maisha ya watu. Tunapofanya dhambi nafsi zetu huwa najisi,pia eneo tulipokuwa wakati tunafanya dhambi hunajisikia pia mf. Kama umefanya dhambi ndani ya ofisi au jengo la kanisa ofisi are jengo Hilo huwa najisi pia na maana ya neno najisi ni kulifanya kilcho hali kuwa haramu kwa hiyo tunapo fanya dhambi tuna ifanya mili yetu na maeneo yetu kuwa haramu mbele za Mungu na njia pekee ya kuvirudisha hivyo Ni Toba nidiyo iageuza kilicho halamu kwa Mungu kuwa halali na huku ikifanha kitu kilekile kuwa halamu kwa shetani.Na dhambi inageuza kilicho halali kuwa halamu kwa Mungu na kulifanya halali kwa ahetani.

Narudia sio tuba inayotuhesabia haki bali Ni Imani katika Kristo.Angali swala la kuwa na mtoto lilifanyika mara moja tangubwakati huo amekuwa mwanao anapokosa haiondoi kuwa sio mwanao hapana bado Ni mtoto wako. Kitendo Cha mtoto Kuja kukuomba msamaha huwa kinarejesha furaha ya baba na pia kitendo Cha baba kumsamehe Mwana hurudiaha Amani ndani ya Mwana Ni kwa njia hii uhusiano Kati ya a mtoto na mzazi huimarika Sana. Ndivyo ilivyo hata kwa baba yetu was Mbinguni, ndiyo maana mahalo flani amesema "nirudieni Mimi kwa mioyo yenu yote".

Mpendwa nalicha swali ulifanyie maamuzi mwenyewe Kama no Toba inakuhusu au haikuhusu Lakini Mimi niwe mkweli kuwa kwangu Mimi Toba Ina nihusu zaidi kuliko hata ndugu ambao bado hawajaamini.

Ufunuo wa Yohana 3:4
[4]Lakini unayo majina machache katika Sardi, watu wasioyatia mavazi yao uchafu. Nao watakwenda pamoja nami hali wamevaa mavazi meupe, kwa kuwa wamestahili.

Ufunuo wa Yohana 7:14
[14]Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo.

Mbarikiwe nyote.
Na. Mal. Samuel

Friday, December 8, 2017

Ushauri juu ya ndoto1.

Samuel

Bwana Yesu asifiwe!!.
Leo tujifunze juu ya ndoto na si lengo la somo hili kukufundisha kutafasiri ndoto bali kukupa tahadhali juu ya ndoto unaozoota na tafasiri unayoyopewa juu ya ndoto. Hii ni kwa sababu ndoto ni kiungo mhimu sana kati ya maisha ya kimwili na yale ya kiroho. Nataka tuangalie mambo machche juu ya ndoto.

Jambo la kwanza
Ndoto ni mlango ambao mingu huitumia kuingiza vitu kwa wanadamu na pia ni lugha ambayo Mungu baba wa Bwana wetu Yesu huitumia kuwasiliana na watu duniania. Ayubu 33:14-15]Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;
Mwanzo 20:3
Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto ya usiku, akamwambia, Umekuwa mfu wewe kwa sababu ya mwanamke huyu uliyemtwaa, maana ni mkewe mtu
 Kwa hiyo Mungu anaweza kutumia ndoto kusema nasi. Lugha ya ndoto ni lugha ya picha kwa sehemu kubwa.

Jambo la pili.
Ukisoma Bible inatuambia wazi kuwa kuna vianzo vitatu vya ndoto ambazo mtu anaweza kuota.

Shughuli Nyingi.
Napenda nikuambie hapa kuwa si wana sayansi waliosema ndoto huja kwa sababu ya shughuli au mawazo uliyokuwa unaweza mchana bali ni Mungu mwenyewe kasema kupitia Bible, tunasoma
Mhubiri 5:3
[3]Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi; na sauti ya mpumbavu kwa njia ya wingi wa maneno. Nataka ujue hili ya kuwa bible ni kitabu kilichoandwa siku Nyingi zaidi kuliko vitabu vingine na kama wana sayansi wamekuja kusema Yale ambayo biblia iliisha yasema kabla basi ni kweli kuwa wao wamenukuu tuu biblia na si kwamba wamegundua.

Chanzo cha pili.
Mungu mwenyewe anahusika na ndoto kwa kuwaletea wanadamu ndoto ili aseme nao katika mambo mbalimbali. Mwanzo 31:11 Na malaika wa Mungu akaniambia katika ndoto, Yakobo! Nikasema, Mimi hapa. Mwanzo 31:11,24 Na alaika wa Mungu akaniambia katika ndoto, Yakobo! Nikasema, Mimi hapa.Mungu akamjia Labani, Mshami, katika ndoto ya usiku, akamwambia, Ujihadhari, usimwambie Yakobo neno la heri wala la shari.

Chanzo cha tatu.
Yeremia 23:32 ".....juu ya hao wanaotabiri ndoto za uongo, asema BWANA, na kuzisema, na kuwakosesha watu wangu kwa uongo wao, na kwa majivuno yao ya upuzi, lakini mimi sikuwatuma, wala sikuwapa amri; wala hawatawafaidia watu hawa hata kidogo, asema BWANA. Kwa hiyo kama Mungu hakuwatuma na bado waliota ndoto inamaana ndoto zao zilitoka mwingine na si kwa Mungu bali kwa slShetani hii ni kwa sababu lengo la ndoto zao ilikuwa kuwasaulisha watu jina la Bwana.

Jambo la tatu.
Tofauti na lugha zingine ambazo msamiati wake hubeba maana ileile yaani haubadiliki,mfano neno “meza” lina maana ya kitu kinachitwa meza au likimaanisha watu kukaa pamoja kwa ajili ya kulizungumzia tatizo lao. Lakini kwa upande wa ndoto ni tofauti kabisa maana ya vitu vinavyo tumika katika ndoto hubadilika badilika kutegemeana na kile Mungu amekusudia kukisema kwa mtu husika, hivyo nakushauri usikalili ndoto.

Mfano.
Mwanzo 37:7
Tazama, sisi tulikuwa tukifunga miganda shambani, kumbe! Mganda wangu ukaondoka ukasimama, na tazama, miganda yenu ikazunguka ikainama mbele ya mganda wangu.
Mwanzo 37:7,9
[7]Tazama, sisi tulikuwa tukifunga miganda shambani, kumbe! Mganda wangu ukaondoka ukasimama, na tazama, miganda yenu ikazunguka ikainama mbele ya mganda wangu.
[9]Akaota tena ndoto nyingine, akawaambia ndugu zake, akasema, Angalieni, nimeota ndoto nyingine; na tazama, jua na mwezi na nyota kumi na moja zikaniinamia.
Unaona hapa yakwba Yuaufu aliota ndoto tofauti zenye kubeba vitu tofauti yaani miganda na nyingine jua na mwezi lakini ndoto zote zilibeba ujumbe mmoja. Ni hatari sana kufasiri ndoto kwa njia ya kukariri vitu vinavyo husika katika ndoto kwani huwezi kupata ujumbe husika na hivyo kupoteza lengo. Nimekuwa nikisoma vitabu na mafundisho juu ya ndoto nilichogundua ni kuwa watumishi wengi hufundisha kufasiri ndoto kwa kuwakaririsha watu kuwa ukiona hili ujue maana yake ni hii, mfano ukiona ng’ombe ujue ni matambiko au ukiona nyoke basi ujue ni uchwai au nguvu za giza. Lakini nikukumbushe tuu kuwa si Mara zote itakuwa hivyo.Faham ya kuwa hakuna alichomba Shetani vitu vyote muumbaji wake ni Mungu mwenyewe japo shetani anaweza kutumia tu, hivyo katika ndoto. Shetani alimtumia myoka katika Edeni sawa, hii haikumzuia Mungu kumtumia alama ya nyoka kwani Musa alimwinua nyoka jangwani.
Hesabu 21:8-9
[8]Bwana akamwambia Musa, Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi.Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi.

Unajua ni kama vile leo speaker ileile inatumika kupiga muziki kule wanaita sijui bilicana Mimi cjui vizuri mtanisahihisha ndiyo hiyohiyo tunaitumia kanisani kuhubiri injili,kule kuitumia kumtukuza shetani hakutuzuii sisi kuitumia kwa utukufu wa Mungu, kwetu sisi tunaangalia ujumbe unatoka kupitia spika na si spika yenyewe. Kadhalika yatupasa tuhangaike na ujumbe unaoletwa kupitia vitu tunavyoona katika ndoto badala ya kuangalia kitu husika.

Jambo la nne.
Ile kwamba baadhi ya ndoto huja kwa sababu ya shughuli Nyingi hakumzuii Mungu kukujibu kupitia ndoto hata hiyo ya mawazo yako,kwani Mungu anaweza kukujibu juu ya maswali uliyo kuwa unajiuliza mchana. Danieli 2:27,29
Daniel I ajibu mbele ya mfalme, akasema, Ile siri aliyoiuliza mfalme, wenye hekima hawawezi kumfunulia mfalme; wala wachawi, wala waganga, wala wanajimu;Wewe, Ee mfalme, mawazo yako yaliingia moyoni mwako kitandani pako ya mambo yatakayokuwa halafu; na yeye afunuaye siri amekujulisha mambo yatakayokuwa.

Ndoto aliyota mfalme ilikuwa ni matokeo ya kile alikuwa anawaza mchana wa siku hiyo,nadhani alikuwa anawaza juu ya ufalme wake itakuwaje akiondoka maana ilikuwa mkubwa mno na Daniel I anasema kuwa Mungu ameamua kumjulisha mawazo ya moyo wake mflme. Naweza kusema ndoto ile ilikuja ili kujibu maswali aliyokuwa mayo mfalme moyoni mwake. Hivyo unaweza ukawa na maswali juu yamambo kadhaa na usipate JIBU au ulawa unamuuliza Mungu naye anaweza kutumia ndoto kukujibu maswali au Maombi yako, usipuuze tu kwa vile ulichoota ni kile ulikuwa unawaza mcha bali jifunze kukaa chini na kutafakari kwa kina juu ya ndoto hiyo.

Jambo la tano.
Si kila ndoto utahitajika kiifuatilia hii ni kwa sababu zingine ni shughuli za mchana tuu, na ili uweze kujua kama ndoto uliyoota ina ujumbe kwako kuna mambo kadhaa yatajitokeza kwako na moja wapo ni ……

Mpendwa muda wangu umeishia hapa leo, naomba tuonane katika somo lijalo nami nitaendelea hapa nilipoishia.Mhimu tuombeane ili tuzidi kutenda kazi yake Mungu baba.Neno inakukaribisha kuomboa na kumobea mumishi ili aseme kilicho cha Mungu na Mungu baba amjalie kukaa uweponi pake daima hata apate luzinena siri za Mungu kwa ujasiri.Ikiwa unabarikiwa na mafundisho haya usiache kusambambaza na wengine wapate na kama utapenda kufuatilia somo hili na mengine mengi usiache kulike ukrasa huu ili uweze kuyapata mafundisho haya mapema zaidi.
Asante.

Sunday, December 4, 2016

Huduma za kijamii

Samuel

Kama huduma Tunawapelekea neno la Mungu watu waishio katika mazingira magumu kama vile yatima, wajane, wafungwa na wazee.Tuna watembekea katika vituo vyao au sehemu wanazo ishi ambapo huwa tunapeleka ujumbe wa Mungu pamoja sadaka zetu hapo kama zawadi  tukifurahi wema wa Mungu pamoja nao.

Tunashiriki huduma zingime za kijamii ikiwa no pamoja na kujitolea kulipia  ada za wanafunzi, kuwanunulia vifaa vya shule, na mengine mengi.


 Karibu tujenge ufalme wa Mungu

Saturday, December 3, 2016

Maomni/maombezi

Samuel

Kutokana na mipaka ya kidini,kidhebu na kimila tunatambua kuwa wapo watu ambao hawawezi kuingia kanisani, jambo hili linawanyima kupokea vipawa vya Mungu wao ikiwa ni pamoja na kumtambua Mungu katika maisha yao.

Neno ministry hutoa huduma ya  maombi,maombezi, mafundisho na ushauri kupitia mtando,kwa njia hii tumewafikia wengi na wamepokea Baraka zao.Huduma za maobi na maombezi pia hutolewa kwa kuonana na mhusika ikiwa atapenda kufanya hivyo.Hiduma hii hutolewa pasipo malipo ya aina yoyote ile.