Showing posts with label Huduma. Show all posts
Showing posts with label Huduma. Show all posts

Sunday, December 4, 2016

Huduma za kijamii

Samuel

Kama huduma Tunawapelekea neno la Mungu watu waishio katika mazingira magumu kama vile yatima, wajane, wafungwa na wazee.Tuna watembekea katika vituo vyao au sehemu wanazo ishi ambapo huwa tunapeleka ujumbe wa Mungu pamoja sadaka zetu hapo kama zawadi  tukifurahi wema wa Mungu pamoja nao.

Tunashiriki huduma zingime za kijamii ikiwa no pamoja na kujitolea kulipia  ada za wanafunzi, kuwanunulia vifaa vya shule, na mengine mengi.


 Karibu tujenge ufalme wa Mungu

Saturday, December 3, 2016

Maomni/maombezi

Samuel

Kutokana na mipaka ya kidini,kidhebu na kimila tunatambua kuwa wapo watu ambao hawawezi kuingia kanisani, jambo hili linawanyima kupokea vipawa vya Mungu wao ikiwa ni pamoja na kumtambua Mungu katika maisha yao.

Neno ministry hutoa huduma ya  maombi,maombezi, mafundisho na ushauri kupitia mtando,kwa njia hii tumewafikia wengi na wamepokea Baraka zao.Huduma za maobi na maombezi pia hutolewa kwa kuonana na mhusika ikiwa atapenda kufanya hivyo.Hiduma hii hutolewa pasipo malipo ya aina yoyote ile.
Samuel

Tunamshukuru Mungu kutujalia neema ya kuyafika maeneo mbalimbali ya nchi yetu kwa ajili ya semina . Semina hizi huandaliwa kwa kushirikiana na umoja wa makanisa au kanisa moja wapo mahali semina hufanyika.

Mara nyingi gharama za kuendesha semina hubebwa na huduma ya Mkate hai ministry isipokuwa ukumbi ambao huwa ni kanisa litakalo pendekezwa na umoja huo au kanisa litakalo shiriki pamoja nasi kuandaa semina.

Pamoja na kufanya semina,pia huduma imekuwa ikitoa watumishi kwenda kuhudumu ibaada za kawaida au kufundisha semina katika kanisa litakalo hitaji Huduma ya mafundisho au mahubiri, huduma hii hutolewa pasipo malipo yoyote