Friday, December 8, 2017

Ushauri juu ya ndoto1.


Bwana Yesu asifiwe!!.
Leo tujifunze juu ya ndoto na si lengo la somo hili kukufundisha kutafasiri ndoto bali kukupa tahadhali juu ya ndoto unaozoota na tafasiri unayoyopewa juu ya ndoto. Hii ni kwa sababu ndoto ni kiungo mhimu sana kati ya maisha ya kimwili na yale ya kiroho. Nataka tuangalie mambo machche juu ya ndoto.

Jambo la kwanza
Ndoto ni mlango ambao mingu huitumia kuingiza vitu kwa wanadamu na pia ni lugha ambayo Mungu baba wa Bwana wetu Yesu huitumia kuwasiliana na watu duniania. Ayubu 33:14-15]Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;
Mwanzo 20:3
Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto ya usiku, akamwambia, Umekuwa mfu wewe kwa sababu ya mwanamke huyu uliyemtwaa, maana ni mkewe mtu
 Kwa hiyo Mungu anaweza kutumia ndoto kusema nasi. Lugha ya ndoto ni lugha ya picha kwa sehemu kubwa.

Jambo la pili.
Ukisoma Bible inatuambia wazi kuwa kuna vianzo vitatu vya ndoto ambazo mtu anaweza kuota.

Shughuli Nyingi.
Napenda nikuambie hapa kuwa si wana sayansi waliosema ndoto huja kwa sababu ya shughuli au mawazo uliyokuwa unaweza mchana bali ni Mungu mwenyewe kasema kupitia Bible, tunasoma
Mhubiri 5:3
[3]Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi; na sauti ya mpumbavu kwa njia ya wingi wa maneno. Nataka ujue hili ya kuwa bible ni kitabu kilichoandwa siku Nyingi zaidi kuliko vitabu vingine na kama wana sayansi wamekuja kusema Yale ambayo biblia iliisha yasema kabla basi ni kweli kuwa wao wamenukuu tuu biblia na si kwamba wamegundua.

Chanzo cha pili.
Mungu mwenyewe anahusika na ndoto kwa kuwaletea wanadamu ndoto ili aseme nao katika mambo mbalimbali. Mwanzo 31:11 Na malaika wa Mungu akaniambia katika ndoto, Yakobo! Nikasema, Mimi hapa. Mwanzo 31:11,24 Na alaika wa Mungu akaniambia katika ndoto, Yakobo! Nikasema, Mimi hapa.Mungu akamjia Labani, Mshami, katika ndoto ya usiku, akamwambia, Ujihadhari, usimwambie Yakobo neno la heri wala la shari.

Chanzo cha tatu.
Yeremia 23:32 ".....juu ya hao wanaotabiri ndoto za uongo, asema BWANA, na kuzisema, na kuwakosesha watu wangu kwa uongo wao, na kwa majivuno yao ya upuzi, lakini mimi sikuwatuma, wala sikuwapa amri; wala hawatawafaidia watu hawa hata kidogo, asema BWANA. Kwa hiyo kama Mungu hakuwatuma na bado waliota ndoto inamaana ndoto zao zilitoka mwingine na si kwa Mungu bali kwa slShetani hii ni kwa sababu lengo la ndoto zao ilikuwa kuwasaulisha watu jina la Bwana.

Jambo la tatu.
Tofauti na lugha zingine ambazo msamiati wake hubeba maana ileile yaani haubadiliki,mfano neno “meza” lina maana ya kitu kinachitwa meza au likimaanisha watu kukaa pamoja kwa ajili ya kulizungumzia tatizo lao. Lakini kwa upande wa ndoto ni tofauti kabisa maana ya vitu vinavyo tumika katika ndoto hubadilika badilika kutegemeana na kile Mungu amekusudia kukisema kwa mtu husika, hivyo nakushauri usikalili ndoto.

Mfano.
Mwanzo 37:7
Tazama, sisi tulikuwa tukifunga miganda shambani, kumbe! Mganda wangu ukaondoka ukasimama, na tazama, miganda yenu ikazunguka ikainama mbele ya mganda wangu.
Mwanzo 37:7,9
[7]Tazama, sisi tulikuwa tukifunga miganda shambani, kumbe! Mganda wangu ukaondoka ukasimama, na tazama, miganda yenu ikazunguka ikainama mbele ya mganda wangu.
[9]Akaota tena ndoto nyingine, akawaambia ndugu zake, akasema, Angalieni, nimeota ndoto nyingine; na tazama, jua na mwezi na nyota kumi na moja zikaniinamia.
Unaona hapa yakwba Yuaufu aliota ndoto tofauti zenye kubeba vitu tofauti yaani miganda na nyingine jua na mwezi lakini ndoto zote zilibeba ujumbe mmoja. Ni hatari sana kufasiri ndoto kwa njia ya kukariri vitu vinavyo husika katika ndoto kwani huwezi kupata ujumbe husika na hivyo kupoteza lengo. Nimekuwa nikisoma vitabu na mafundisho juu ya ndoto nilichogundua ni kuwa watumishi wengi hufundisha kufasiri ndoto kwa kuwakaririsha watu kuwa ukiona hili ujue maana yake ni hii, mfano ukiona ng’ombe ujue ni matambiko au ukiona nyoke basi ujue ni uchwai au nguvu za giza. Lakini nikukumbushe tuu kuwa si Mara zote itakuwa hivyo.Faham ya kuwa hakuna alichomba Shetani vitu vyote muumbaji wake ni Mungu mwenyewe japo shetani anaweza kutumia tu, hivyo katika ndoto. Shetani alimtumia myoka katika Edeni sawa, hii haikumzuia Mungu kumtumia alama ya nyoka kwani Musa alimwinua nyoka jangwani.
Hesabu 21:8-9
[8]Bwana akamwambia Musa, Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi.Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi.

Unajua ni kama vile leo speaker ileile inatumika kupiga muziki kule wanaita sijui bilicana Mimi cjui vizuri mtanisahihisha ndiyo hiyohiyo tunaitumia kanisani kuhubiri injili,kule kuitumia kumtukuza shetani hakutuzuii sisi kuitumia kwa utukufu wa Mungu, kwetu sisi tunaangalia ujumbe unatoka kupitia spika na si spika yenyewe. Kadhalika yatupasa tuhangaike na ujumbe unaoletwa kupitia vitu tunavyoona katika ndoto badala ya kuangalia kitu husika.

Jambo la nne.
Ile kwamba baadhi ya ndoto huja kwa sababu ya shughuli Nyingi hakumzuii Mungu kukujibu kupitia ndoto hata hiyo ya mawazo yako,kwani Mungu anaweza kukujibu juu ya maswali uliyo kuwa unajiuliza mchana. Danieli 2:27,29
Daniel I ajibu mbele ya mfalme, akasema, Ile siri aliyoiuliza mfalme, wenye hekima hawawezi kumfunulia mfalme; wala wachawi, wala waganga, wala wanajimu;Wewe, Ee mfalme, mawazo yako yaliingia moyoni mwako kitandani pako ya mambo yatakayokuwa halafu; na yeye afunuaye siri amekujulisha mambo yatakayokuwa.

Ndoto aliyota mfalme ilikuwa ni matokeo ya kile alikuwa anawaza mchana wa siku hiyo,nadhani alikuwa anawaza juu ya ufalme wake itakuwaje akiondoka maana ilikuwa mkubwa mno na Daniel I anasema kuwa Mungu ameamua kumjulisha mawazo ya moyo wake mflme. Naweza kusema ndoto ile ilikuja ili kujibu maswali aliyokuwa mayo mfalme moyoni mwake. Hivyo unaweza ukawa na maswali juu yamambo kadhaa na usipate JIBU au ulawa unamuuliza Mungu naye anaweza kutumia ndoto kukujibu maswali au Maombi yako, usipuuze tu kwa vile ulichoota ni kile ulikuwa unawaza mcha bali jifunze kukaa chini na kutafakari kwa kina juu ya ndoto hiyo.

Jambo la tano.
Si kila ndoto utahitajika kiifuatilia hii ni kwa sababu zingine ni shughuli za mchana tuu, na ili uweze kujua kama ndoto uliyoota ina ujumbe kwako kuna mambo kadhaa yatajitokeza kwako na moja wapo ni ……

Mpendwa muda wangu umeishia hapa leo, naomba tuonane katika somo lijalo nami nitaendelea hapa nilipoishia.Mhimu tuombeane ili tuzidi kutenda kazi yake Mungu baba.Neno inakukaribisha kuomboa na kumobea mumishi ili aseme kilicho cha Mungu na Mungu baba amjalie kukaa uweponi pake daima hata apate luzinena siri za Mungu kwa ujasiri.Ikiwa unabarikiwa na mafundisho haya usiache kusambambaza na wengine wapate na kama utapenda kufuatilia somo hili na mengine mengi usiache kulike ukrasa huu ili uweze kuyapata mafundisho haya mapema zaidi.
Asante.

Samuel

Author & Editor

Mimi si mchungaji au nabii bali ni mjumbe tu wa Mungu ambaye kwa neema yake amenitumwa kwa kizazi hiki niwaambie habari zake Mungu na falme wake,nami nakuombea Mungu akujalie neema ya kuelewa na kuyaweka katika matendo uliyo yasoma.