Thursday, December 19, 2019

Samuel
IdeaPad ni moja wapo ya bidhaa inayo tengenezwa na kampuni ya Lenovo inayojishughulisha na utengenezaji wa kompyuta ikiwemo Ideapad s125. kama ilivyo Kwa bidhaa nyingine kadhalika IdeaPad s145 ipo sokoni, inapatikana Kwa urahisi katika nchi nyingi duniani kupitia mtandao wa Amazon. Ukitazama tu bei yake utapata tariifa flani kuhusu Lenovo s145. Kama uonavyo bei yake ni ya chini Kwa hiyo usitegemee laptop hii kumfanya majukumu mazito ya kikompyuta kwani imeundwa maalumu Kwa ajili ya kazi za kawaida na si vingine, hata hivyo haina maana kuwa haiwezi kumfanya majukumu mazito unaweza lakini si Kwa ufanisi mkubwa, ushauri wetu wa bure ni vema itumike katitka majukumu ya kawaida.

Full story.

Design

Laptop hii ni mzuri na ya kuvutia Sana kuitazama, ni nyepesi na ina uzito usio zidi 1.45Kg pia ni nyembamba. Sifa hizi huifanya uweze kwenda nayo mahali popote bila kuhisi kama kuna kitu umebeba mgongoni kwako. Siku hizi nasikia unapo nunua unapata na begi lake bure, unaweza kupata tarifaa kamaili kuhusu mabegi ya Lenovo Kwa kuongia hapa.

Processor

Lenovo IdeaPad s145 inatumia celeron or pentium processor, Kwa mantiki hiyo huwezi run demanding Apps au kumfanya majukumu mazito ya kikompyuta kama nilivyo Sema hapo awali. Lakini kwa mtumiaji wa kawaida hii ni laptop mzuri sana ambayo huhitaji kuvunja bank yote ili uweze kuipta Laptop hii,inafaa Sana hasa Kwa waanafunzi ukiondoa Wale wa kozi za engineering na multimedia ambao wakati mwingine huhitaji high resolution au run demanding Apps.

Display

Ingawa display yake ni kubwa (15.6inch) ambyo ni display nziuri Kwa matumizi kama kuangalia movie au kucheza game (gaming), ukweli ni kwamba display hii ina tatizo la resolution Kwani ina resolution 1366x768 ambayo si resolution nziuri Kwa matumizi ya gaming hata ukiiangalia viewing angle yake si nziuri.

Sound


CPU.

Ingawa kuna uwezekano wa upgrade toka IdaPad ya kawaida na kuwa kama Toleo la gharama la IdeaPad 145 inayo tumia i7 processor inayo kupa rocket boosting speed,hasara yake ni kwamba utalazimika kulipa zaidi na mwisho wa   siku  bado unapambana na matatizo kadhaa ikiwemo poor resolution na pia kuna uwezekano wa  battery yako uwezo wake kushuka Sana.

Storage.

Laptop mpya inakuja storage ya 1TB, hii ni habari njema Sana Kwa kuwa Una kuwa umepata storage kubwa utakayo weza kukidhi matumizi yako. Habari mbaya no kwamba ina 5400rpm hard disk Jambo linalo ifanya loading time yake kuwa ndefu hasa unapotaka run Apps au kutafuta mafaili.Kumbuka kuwa inawezekana kuupgrade speed yake wewe mwenyewe nyumbani Kwa kwako Kwa kufungua screw chache na kupachika RAM mpya lakini tunapenda kushauri usifanye hivyo watagute watu wenye uzoefu wakusaidie ikiwa unawazo la kuiongezea speed laptop yako.

Bottom line.

katika uchunguzj wetu tumebaini kuwa Laptop hii ni mzuri ukilinganisha na bei yake. Hivyo tuna shauri kwa mtumiji wa kawaida no vema ukajipatia Lenovo s145 utaokoa pesa yako na bado ukafanya kazi zako Kwa ufanisi mkubwa. Tuna amini hutasita  kutushukuru baadaye. Inapatikai maeneo mengi na moja wapo ni katika Amazon  ambapo kwetu ni mahali salama kabisa kwa manunuzi yako, on purchase Laptop hii inakuja na adapter yake lakini pia unaweza kujipatia vifaa vingine mhimu katika kuboresha utendaji wa Laptop yaka kama vile external memory na vingine ambavyo unaweza kubapata Kwa gharama nafuu kupitia kiungo hiki Lenovo s145 accessories.

Sunday, December 8, 2019

Mchungaji mwema

Samuel

Shalom kanisa!
Mchungaji mwema:
Leo naomba tuangalie  neno hili la mchungaji.yupo mchungaji mwema wa Roho za watu na mchungaji mwema wa
ng'ombe. Nami nataka tumwangalie yule wa ng'ombe tupate kuelewa vema.

Ni jukumu la Mchungaji wa ng'ombe huyu ndiye anaye jua wapi mifugo yake itapata malisho lakini ng'ombe(mifugo) wenyewe hawajui, huwa anafanya bidii kuwaongoza  g'ombe wake wafuate njia lakini ng'ombe wenyewe hawajui njia. Mchungaji wa ng'ombe yeye hujua sana afya ya mifugo wake. Kwa kweli ng'ombe humtegemea yeye kwa kila kitu.

Nimepata kutafakari juu ya ng'ombe nilipo kuwa nikisoma maneno haya 

John 10:1-5
[1]Verily, verily, I say unto you, He that entereth not by the door into the sheepfold, but climbeth up some other way, the same is a thief and a robber. 
Yesu aliwaambia, Amin, amin, nawaambieni, Yeye asiyeingia mlangoni katika zizi la kondoo, lakini akwea penginepo, huyo ni mwivi naye ni mnyang’anyi.
[2]But he that entereth in by the door is the shepherd of the sheep. 
Aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo.
[3]To him the porter openeth; and the sheep hear his voice: and he calleth his own sheep by name, and leadeth them out. 
Bawabu humfungulia huyo, na kondoo humsikia sauti yake; naye huwaita kondoo wake kwa majina yao, na kuwapeleka nje.
[4]And when he putteth forth his own sheep, he goeth before them, and the sheep follow him: for they know his voice. 
Naye awatoapo nje kondoo wake wote, huwatangulia; na wale kondoo humfuata, kwa maana waijua sauti yake.
[5]And a stranger will they not follow, but will flee from him: for they know not the voice of strangers. 
Mgeni hawatamfuata kabisa, bali watamkimbia; kwa maana hawazijui sauti za wageni.

Kwa kweli nikawa silewi ndipo nilipoomba msaada wa Roho Mtakatifu anisaidie kuelewa, baada ya ombi hili nikaletewa picha ya ng'ombe na ndiyo sababu mimetumia ng'ombe badala ya kondoo.

Sasa twende pamoja, Yesu ndiye mchungaji mwema , Japo si neno njema lakini nakuomba ukae mahali pa ng'ombe upate kuelewa vema

Unajua ng'ombe ni msumbufu sana kwa kuwa hajui atakula wapi hivyo mchungaji ng'ombe tu ndiye ajuye na huamua wapi ampeleke ng'ombe wake akale hata hivyo ng'ombe hafuati njia bali hutoka katika njia na kutaka kula mazao ya watu mchungaji wa ng'ombe hulazimika kumkataza asiharibu mazao ya watu kwa kuwa anakompeleka kuna malisho bora ya hayo lakini ng'ombe haelewi na hukasirika.

Hivi ndivyo tulivyo,hatujui kesho yetu wala ridhiki zetu zilipo ni Mungu pekee ajuauye naye hutuongaza palipo malisho mema.

Psalms 23:2
[2]He maketh me to lie down in green pastures: he leadeth me beside the still waters. 
Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza.

Hata hivyo hatuelewi tunakimbilia mambo mengine nje ya njia ya Mungu ( kusudi ) mbaya zaidi hata akitutaza tunakasirika! Eeh Yesu turehemu.

Ng'ombe hajui hata kusafisha mahali anapolala ni kazi ya mchungaji wa ng'ombe kusafisha zizi lakini wakati mchungaji wa ng'ombe anasafisha banda(zizi), ng'ombe mwenyewe wakati mwingine hupinga mateke kumbe usafi ule ni kwa faida yake, nasi ndiyo tulivyo Roho wa Mungu  anapotaka kutusafisha tuwe safi kusudi uchafu ( dhambi ) usije tuletea maradhi kisha kifo tunakasirika na kumsimanga Kwa maneno magumu ya kweli na sharau kuu.

Romans6:23
[23]For the wages of sin is death; but the gift of God is eternal life through Jesus Christ our Lord. 
Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu. Yesu tuhurumie.

Yesu ni mchungaji mwema huingia mlangoni na mifungo yake humfurahia naye huwafungulia mlango humfuta,naam Yesu ni mchungaji Wa kweli ndiyo maana huja kwako kwa upole na kukueleza juu ya kusudi lake umtumikie wala hakulazimishi umtumikie.

Revelation 3:20
[20]Behold, I stand at the door, and knock: if any man hear my voice, and open the door, I will come in to him, and will sup with him, and he with me. 
Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.

Bali shetani kwa kuwa ni mwizi haipiti mlangoni ndiyo maana anakulazimisha ufanye atakayo wala hakuombi. Changua leo kuwa upande Wa mchungaji mwema au mwizi, lakini sisi Neno ministry tunakushauri chagua upande wa  Yesu.

Nataka ufahamu leo kuwa kama ilivyo kwa mchungaji wa ng'ombe, ndiyo ilivyo kwake Yesu mchungaji mwema,hujishughuliaha sana ili kuhakikisha unapata malisho nyakati zote.
Psalms 23:5
[5]Thou preparest a table before me in the presence of mine enemies: thou anointest my head with oil; my cup runneth over. 
Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika.

Ndiyo usiogope ana Huruma sana namfahamu vizuri kwani amesema mwenyewe kuwa

John 6:37
[37]All that the Father giveth me shall come to me; and him that cometh to me I will in no wise cast out. 
Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe.

Kama ilivyo kwa ng'ombe wala hajui atakula wapi kesho wala atatibiwa na  nani lakini yeye siku zote humwamini bwana wake wake atampeleka palipo na na malisho pia hata bwana wake akichelewa hupiga kelele kuomba msaada apelekwe panapo malisho.

Kadhalika nawe weka Imani yako kwa Yesu kuwa atakupa unacho hitaji hata kikichelewa piga kelele kwa njia maombi atakuja na kukupa hitaji lako.

Jifunze kumsubili Mungu anaye JIBU maombi hata kama litachelewa ujue ni kwa faida yako limechelewa au haja kupa.

Ushuhuda.
Mimi mwenyewe ni mtu niliyepata Neema ya kwenda shule ya juu, nakumbuka wakati naenda chuo mara ya kwanza niliomba mkopo sikupata japo nilikuwa na sifa zote za kupata mkopo, nilikasirika sana kwa nini Mungu hakurusu nipate mlopo. Japo hakunipa sababu lakini alinisaidia kuendelea na masomo yangu na nilifanikiwa kumaliza. Nilirudi chuoni tena na nikaomba mkopo lakini pia si kupata hapo nilazidi kuchukia na kumchukia sana Mungu, Mungu akaa kimya asinijibu why. Kwa shida Sana nilifanikiwa kumaliza chuo. Baada ya kurudi mtaani nikaaa miaka mingi bila kuwa na kazi ya maana, siku moja rafiki yangu akaniambia anadaiwa million 15 na bodi ya mikopo deni limejilimbikiza. Usiku ule nikitafakari juu ya deni la rafiki yangu ndipo Roho Wa Yesu akaniambia "Je ninge kupa ule mkopo ungelipaje?. japo ulinikasirikia sana lkn nilijua yaliyoko mbele yako nikazuia usipate mkopo kwa kuwa nakuwazia mema"

Jeremiah 29:11
[11]For I know the thoughts that I think toward you, saith the LORD, thoughts of peace, and not of evil, to give you an expected end. 
Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.

Hapo ndipo nilipo jua kuwa mawazo mema ya Mungu ni tofauti na vile ninvyo fikiri Mimi, tangu siku hiyo nimejua kuwa kila alifanyalo Yesu kwangu ni jema hata kamaa lina maumivu kwangu najua amelifanya kwa kuwa ni njema machoni pake na hii ni kwa ajili ya faida yangu.

Mpendwa hakuna mchungaji mwema anayeitakia mifungo yake madhara Bali yeye yu tayari kuutoa uhai wake kwa ajili ya mfugo wake.hivi ndiyo Yesu afanyanyvo kwako.akikuzuia jambo usikasirike Bali mshukuru kwa kuwa amefanya hayo kwa faida yako.

Kumbuka kuwa mawazo yetu si yake Mungu na tena mazo yake yako juu sana kuliko mawazo yetu.

Katika yote fahamu kuwa anakuwazia mema wala so mabaya.