Saturday, December 8, 2018

Nani aombe toba?.

Samuel

Shalom kanisa!.
Leo napenda tutazame japo kidogo juu ya toba kwa sababu ya ufinyu wa ukrasa wetu huu,tutaangalia mambo machache tuu Lakini nikiamni Roho wa Bwana atakuwezesha kujifunza ktk muda wako wa spare.

Toba kwa lugha nyepesi kabisa Ni kugeuka yaani kumgekukia Mungu wako na tunaposema kuomba Toba Ina maana ya kufanya maombi ya kutaka  kumsihi Mungu atusaidie tumgeukie yeye katika maisha yetu haya.

Nimezigawa Toba ktk mafungu mawili:

Moja:
Ni Toba inayofanyika unapokoka au unampokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako Toba hii Ni zao la Roho mtakatifu. Tunasoma kuwa 

2 Wakorintho 7:10
[10]Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba liletalo wokovu lisilo na majuto; bali huzuni ya dunia hufanya mauti.

Toba ile tulioimba wakatu tunamkiri kristo haikutokana na ushawiashi wa mwanadamu Bali ilikuwa kazi ya Roho Mtakatifu iliyofanyika ndani ndiyo iliyotuo goza hata tukamkri Kristo na hata tukapokea kipawa Cha wakovu.

Warumi 10:9-10
[9]Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.
[10]Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.

Ni tendo linapofanyika mara moja mtu husamehewa dhambi na kuhesabiwa haki na kumpokea wokovu, huanza Toba, Kisha hufuata kusamehewa dhambi,kuhesabiwa haki na Kisha kupata wokovu.

Mhimu kujua kuwa sio Toba inayotuhesabia haki bali ni Imani katk krsto Yesu, Mungu anaiona hiyo Imani ndani yetu hutuhesabia haki bure kwa njia ya neema maana neema ni kitu mtu hupewa bure pasipo kuifaniya kazi 

Warumi 4:4-5
[4]Lakini kwa mtu afanyaye kazi, ujira wake hauhesabiwi kuwa ni neema, bali kuwa ni deni.
[5]Lakini kwa mtu asiyefanya kazi, bali anamwamini yeye ambaye amhesabia haki asiyekuwa mtauwa, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki.

Toba hii tukiomba ikiwa na lengo la kusihi Mungu atusikie kilio chetu kuwa tumetambua kuwa tuko mbali na uwepo wake katika maisha yetu na kwamba Sasa tunamwitaji yeye awe kiongozi katika maisha yetu zaidi Sana tupewe neema ya kuingia katika ufalme wake 

Mbili:

Ile kwamba umeoka haina maana kuwa umefika Mbinguni hapana Bali unapewa tiketi ya kuingia ktk ufalme wa pendo la Mwana wake yaani ufalme wa Mungu. Ndiyo kwanza unaza safari ya kuelekea uzimani, kwa hiyo usifikiri Ni kazi rahisi ni ngumu kusafiri ktk njia hii. Hii Ni kwa sababu njiani utakutana na mtu mwe hasira sana

1 Petro 5:8
[8]Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.

Anatafuta Sana wa kunijaribu na anajitahidi kwa kweli kuhakikisha amekuweza kabisa si njia rahisi hii 

Ufunuo wa Yohana 12:10
[10]Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.

Lengo lake kuu apata Cha kukushitaki mbele za Mungu yaani asipo pata huumia Sana maana ndiyo kazi yake. Kwa hiyo usijaribu kumwona shetani Kama nidiyo chanzo kuasi kwako nakwambia mwezio alikuwa kazini apate Cha kusema.kwa hiyo Jifunze kuwambia kweli baba kuwa umemkosea akusamehe na sio visingizio juu ya ahetani au kusema Ni kwa sababu ya udhaifu was mwili hapana kwani Mungu alipokuambia usitende dhambi alikuwa anajua kabisa kuwa una mwili wa udhafu napia alijua shetani yupo duniani. Visingizio havitatusaidia tukumbuke visingizio vya Adamu havikumsadia kitu.

Ndugu yetu Paulo aliliona Hilo kwamba pamoja na kuwa mwongofu bado alikuwa katika mapambano ya dhambi yaliyo sababishwa na mwili wake mwenyewe amesema

Warumi 7:15-24
[15]Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda.
[16]Lakini kama nikilitenda lile nisilolipenda, naikiri ile sheria ya kuwa ni njema.
[17]Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu
[18]Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati.
[19]Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo.
[20]Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.
[21]Basi nimeona sheria hii, ya kuwa kwangu mimi nitakaye kutenda lililo jema, lipo lililo baya.
[22]Kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani,
[23]lakini katika viungo vyangu naona sheria iliyo mbali, inapiga vita na ile sheria ya akili zangu, na kunifanya mateka ya ile sheria ya dhambi iliyo katika viungo vyangu.
[24]Ole wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?

Mara kadha utu wetu wa ndani unatamani sana kufanya yaliyo ya Mungu lkn mwili hutupinga na tunajikuta tumefanya lile tunalo lichukia. Biblia ipo wazi hapa kuwa ikiwa tunalifanya tusilo lipenda basi dhambi iliyo ndani ya miili yetu ndiyo inayoa sabibisha 
Iwe hivyo. Fahamu kuwa miili yetu inaitikia kwa urahii zaidi mambo ya dunia kuliko ya Mungu hii ndiyo vita kubwa tuliyo waamini kuliko hata kupambana na nguvu za giza, tunasoma kuwa

Mhubiri 7:20
[20]Bila shaka hakuna mwanadamu mwenye haki hapa duniani, ambaye afanya mema, asifanye dhambi.

Ni kwa mantiki hiyo Mungu anatambua ugumu safari yetu ndiyo maana aliruhu iwepo toba tunapo anguka ktk hila za jamaa huyu.Biblia inatutaka kila wakati tuombe Toba mara tuangukapo dhambini. Tunasoma

1 Yohana 2:1-2
[1]Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki,
[2]naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote.

Biblia Inatuagiza tufanye bidii tusianguke dhambini kabisa,hata hivyo inatuambia kuwa ikitokea tumeanguka haraka tukumbuke kwenda kwa Yesu kuomba Toba yaani kusamehewa dhambi zetu kwa kuwa yeye ndiye mpatanishi Kati yetu na Mungu. Soma  vizuri inasema dhambi zetu yaani waamini na za ulimwengu yaani wasio amini.

 Ni kwa kutambua hilo Yohana  ansema
1 Yohana 1:8-10
[8]Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.
[9]Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.
[10]Tukisema kwamba hatukutenda dhambi, twamfanya Yeye kuwa mwongo wala neno lake halimo mwetu.

Angalia tuziungama dhambi zetu yaani sisi yeye ni mwanifu na wa haki atatusafisha, Jua imepasa tuungame yaani tusema samahani  tumekosa mbele zako, tuonyeshe kwa dhati kwamba tumesigitishwa na tulio yafanya,kuwa tunayachua hayo,kuwa hatuyataki, Yesu huisikia Toba yetu Kisha huenda mbele za baba yake kutuombea msamaha.

Mfano 1.
Kanisa la efeso liliwahi kupotoka katika njia yake ya kwanza (upendo) na kujikuta lipo katika nja mpya,Yesu alilikemea kwa kulitaka litubu mara moja

Ufunuo wa Yohana 2:5
[5]Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu.

Kwa hiyo tuba katika maisha ya mwamini Ni mhimu Sana kwa kuwa dhambi ni uchafu was kiroho. Katika ulimwengu Ni vigumu kutochafuka hata ukijifungia chumbani utajikua unachafuka tuu na vumbibhivyo lazima uoge uwe safi.kadhalika dhambi hutja hata Kama umjifungia nyumbani mwako bado dhambi itakujia tuu kwa kuwa dhambi haitoki nje tuu Bali wakati kwingine hutoka katika mawazo ya mioyo yetu.hivyo Ni mhim kwetu kila wakati kwenda ziwani mwa damu ya Yesu tukaoge tuwe Safi ili tuweze kusimama mbele za baba yetu was Mbinguni kwa ujasiri mkuu vinginevyo tutajificha tuu Kama Adamu kwani tutaona aibu ya uchi wetu kiroho 

JUA HILI PIA
Tuomba Toba pia ili tusipatwe na madhara yatokanayo na dhambi

Jambo unalopaswa kujua pia Ni Hili kuwa ikiwa tutatenda dhambi Mungu hafurahishwi nasi kwa hiyo huamua kuturudi kusudi tusipotee kabisa.

Waebrania 12:6-13
[6]Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, 
Naye humpiga kila mwana amkubaliye.
[7]Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye?
[8]Basi kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali.
[9]Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawastahi; basi si afadhali sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi?
[10]Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake.
[11]Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani.
[12]Kwa hiyo inyosheni mikono iliyolegea na magoti yaliyopooza,
[13]mkaifanyie miguu yenu njia za kunyoka, ili kitu kilicho kiwete kisipotoshwe, bali afadhali kiponywe.

Biblia inatuambia kuwa ili kusiwepo kurudia kwa kuwa kurudiwa ndani yake Kuna adhabu ambayo sio kitu Cha kufurahia, basi tukaifanye miguu yetu imara ( isihame katka nja iliyo sawa) ili kufanya njia iliyonyoka ili kilicho kiwete ( kisicho faa) kinyoshwe

Mfano 1.

2 Samweli 12:13-14
[13]Daudi akamwambia Nathani, Nimemfanyia BWANA dhambi. Nathani akamwambia Daudi, BWANA naye ameiondoa dhambi yako; hutakufa.
[14]Lakini, kwa kuwa kwa tendo hili umewapa adui za BWANA nafasi kubwa ya kukufuru, mtoto atakayezaliwa kwako hakika yake atakufa.

Daudi alipo mwambia Nathani nimefanya dhambi unaona jibu la Nadhani Ni Hili Mungu ameiondoa dhambi yako. Unaona hapa jibu Hilo halikuwepo kabla Daudi hajakiri kumtenda Mungu dhambi na usifikiri kuwa Daudi hakujua kuwa alilo fanya Ni dhambi alijua na ndio maana alitaka kuficha iwe Siri.Mtoto alikufa si kwa sababu ametenda dhambi hapana bali ni matokeo ya dhambi ya Daudi. Ni Toba pekee inayo weza kuzuia madhara ya dhambi.kumbuka Toba ya Musa juu ya Israel walipo abudu ndama.

Na HILi
Toba Ina mpa kibari Mungu kuwa upande wako au eneo unaloombea Toba. Fahamu kuwa ulimwengu wa Roho ni ulimwengu unaongozwa kwa sheria.maandiko yanatuambia

Warumi 8:2
[2]Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.

Kwa hiyo ipo Sheria ya uzima na ndiyo inampa Mungu uhali wa kuwepo au kushughulikia Jambo flani katika maisha ya wanadamu,Sasa hii haimanishi kuwa hawezi kufanya chochote mpaka vigezo vya Sheria hii vitimia kumbuka yeye  juu ya Sheria zote anaweza lkn hii Ni nje ya utaratibu alio jiwelea. 

Usisahau kuwa shetani anafanya kazi ktk mnyororo was dhambi Ni Sheria ya dhambi inayompa shetani kibari Cha kutawala maisha ya watu. Tunapofanya dhambi nafsi zetu huwa najisi,pia eneo tulipokuwa wakati tunafanya dhambi hunajisikia pia mf. Kama umefanya dhambi ndani ya ofisi au jengo la kanisa ofisi are jengo Hilo huwa najisi pia na maana ya neno najisi ni kulifanya kilcho hali kuwa haramu kwa hiyo tunapo fanya dhambi tuna ifanya mili yetu na maeneo yetu kuwa haramu mbele za Mungu na njia pekee ya kuvirudisha hivyo Ni Toba nidiyo iageuza kilicho halamu kwa Mungu kuwa halali na huku ikifanha kitu kilekile kuwa halamu kwa shetani.Na dhambi inageuza kilicho halali kuwa halamu kwa Mungu na kulifanya halali kwa ahetani.

Narudia sio tuba inayotuhesabia haki bali Ni Imani katika Kristo.Angali swala la kuwa na mtoto lilifanyika mara moja tangubwakati huo amekuwa mwanao anapokosa haiondoi kuwa sio mwanao hapana bado Ni mtoto wako. Kitendo Cha mtoto Kuja kukuomba msamaha huwa kinarejesha furaha ya baba na pia kitendo Cha baba kumsamehe Mwana hurudiaha Amani ndani ya Mwana Ni kwa njia hii uhusiano Kati ya a mtoto na mzazi huimarika Sana. Ndivyo ilivyo hata kwa baba yetu was Mbinguni, ndiyo maana mahalo flani amesema "nirudieni Mimi kwa mioyo yenu yote".

Mpendwa nalicha swali ulifanyie maamuzi mwenyewe Kama no Toba inakuhusu au haikuhusu Lakini Mimi niwe mkweli kuwa kwangu Mimi Toba Ina nihusu zaidi kuliko hata ndugu ambao bado hawajaamini.

Ufunuo wa Yohana 3:4
[4]Lakini unayo majina machache katika Sardi, watu wasioyatia mavazi yao uchafu. Nao watakwenda pamoja nami hali wamevaa mavazi meupe, kwa kuwa wamestahili.

Ufunuo wa Yohana 7:14
[14]Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo.

Mbarikiwe nyote.
Na. Mal. Samuel