Karibuni

Tunayo furaha Sana kuona mpendwa wetu umetutembela hapa ndani katika website hii ya Meno ministry, Kwa kweli tunanadhamini Sana uwepo wako pamoja nasi hapa ndani siku hii ya leo. Tumekusanyika hapa watu wa mataifa yote tunao amini katika nauti ya Yesu Kristo na katika Roho wake ili kumpa Mungu utukufu ambaye ahadi zake ni Amina na kweli kama tusomavyo katika 2Corintho1:20.

Huduma hii inaami katika Kristo Yesu ambaye ni msingi wa upendo kwa watu wote. Mwongozo
 wetu u katika mafundisho ya kweli ya Biblical na ufunuo halisi wa Roho wa Mungu usio kinzana na neno lake.

Tumekusudia Kwa msaada wa Roho mtakatifu kuwajenga Wana wa Mungu Wanaume Kwa wanawake  waaminio ili waweze kumtumikia Mungu wao Kwa uaminifu.

Tuna mtukuza Mungu Kwa kuyaweka katika matendo mafundisho ya Biblia, maombi, maombezi na kujitoa kwa ajili ya wengine.  Tunamshukuru Sana Mungu ambaye Kwa njia hii amezidi  kujitukuza ndani ya huduma hii Kwa kufanya kazi kuu na za ajabu machoni petu kupitia watumishi wake.

Lego letu ni kuwasaidia waamini kukua hata kufikia kiwango cha ukomavu kiimani bila kujali dhebu la mtu, kwetu mhimu ni kuona kila aminiye katika Kristo Yesu anakuwa kiroho na kuwa mtu aliye komaa kiroho ili asiweze kuyumbishwa na mafundisho ya mpinga Kristo yaliyo enea kila mahali.

Kama unataka kuzidi kukua kiroho basi Neno ministry ni mahali sahihi pa kukata kiu yako ya kiroho.karibu tujifunze neno la Mungu pamoja.

Ubarikiwe